.

Showing posts with label ujumbe. Show all posts
Showing posts with label ujumbe. Show all posts

MELI YAZANA ZANZIBAR


Waokowaji wamefika eneo la tukio

Mv Karama ikiwa abiria 200 tayari juhudi za kuwaokowa wahanga wa meli hiyo zimeanza na tayari mamlaka husika zimeanza kuchukuwa hatuwa za kuwaokowa ikishirikiana na kampuni mbali mbali za usafiri wa baharini.

Muandishi wa ITV Farouk Karim akiwa katika eneo la tukio ameeleza kuwa ameona life jacket zikieleya majini zikiwa hazina watu na baadhi ya vifaa, na mtu mmoja ameokolewa akiwa hai.

TANGAZO KWA UMMA

Karibu SK NETWORK
SK NETWORK ni moja ya mtandao mkubwa na maarufu  hapa nchini Tanzania unaojihusisha na utoaji wa huduma za promotion mitandaoni ikiwa na uzoefu wa miaka mitatu.
Sasa kuanzia tarehe (05/07/2012) tunatoa ofa ya kutangaza matangazo mawili ya biashara yako bure ndani ya mtandao wetu kila mwenzi.
Vigezo
1.       Video:Lazima liwe kwenye youtube kwanza.
2.       Picha:Picha zisizidi tatu.
3.       Words:isizidi kurasa moja (1)

K.K: SK NETWORK haina muda wa kurekebisha kazi yako hivyo basi isome zaidi ya mara moja kabla hujatutumia.
Tembelea blog zetu Kila Siku:
·         www.tanzaniamenu.blogspot.com
·         www.masokoni.blogspot.com
·         www.totolabongo.blogspot.com
·         www.maktabayetu.blogspot.com

          KAULI MBIO YETU: ((TUNATANGAZA, UNAUZA))
Itume hii taarifa hii kwa mtu yeyote mwenye  Biashara.


Wasiliana nasi: +255 713592224, +255767592224
 Barua pepe:sknetwork@live.com,sokonikariakoo@gmail.com

ASANTE.

tembelea blog yetu ya fashion


huwezi ukapata sehemu nyingine vitu adimu kama hivi ni chimbo moja tu hapa tanzania na afrika mashariki na kati...www.totolabongo.blogspot.com...ndo kuna madini ya ukweli ya fashion kaa nasi hiyo ndo blog mama ya SK NETWORK upande wa fashion...

CHINA WAITEKA SABA SABA

 MAONYESHO YA 36 YA SABA SABA......



KIJANA CHUI HUYO......
leo mdau ya SK NETWORK  ilikuwa  saba saba akifwatilia mambo ya fulani fulani katika banda moja wapo maeneo hayo..katika ripoti yake mdau wetu amekiri kuwa sabasaba ya sasa imekuwa na bidhaa nyingi sana za kutoka china .mpaka bidhaa zili ambazo tumezoea kuziona kwa wajasiliamali wa kawaida kabisa kutoka sido na wachina pia wanazo..ingawa si vibaya lakini kwa maono yake na wadau wachache waliohojiwa wamekiri kuwa china inanguvu kubwa ya matangazo na wanaummoja kutuzidi watanzania kiasi kwamba wanapata watazamaji wengi kuliko hata mabanda mengine ya bidhaa za aina kama yao...mabanda ya watanzania sasa  wengi wao  wamekutwa wakiwa wemenyongonyea na wengine hawakaribishi hata wateja..na pia mpangilio wa bidhaa zao hauvutie mteja kuangalia mara mbili... kama kweli tunahitaji kuwa  kwenye ushindani wa biashara na mataifa mengine kama Kenya na China ...basi inabidi tubadilike tuache kuweka vinyago na makatuni mlangoni wakichekesha wateja,,,bali tujitahidi kuweka bidhaa ,mabango ya kuvutia na  wahudumu wachangamfu.Benki fulani fulani zimechukua vijana na kuwaweka barabaran kuhamasisha wateja  jambo hilo si baya bali vijana hao muda mwengine wanageuka usumbufu pale unapokubali kuzungumza nao....Tembeleeni saba saba ya mwaka huu na uje na maoni yako na sisi tutayaweka hewani...











katuni


mgomo wa walimu wapingwa na serekali


kauli ya walimu ya kutangaza mgomo kuanzia tarehe 5 mwenzi.na kuwataka walimu nchi zima kuwaunga mkono katika mgomo wao ambao utafanyika tarehe 5 kama tu serekali itakuwa aija timiza matakwa ya walimu ya kuongezewa mshahara,kuboreshewa mazingira ya kufanya kazi na kuwapa motivation walimu wale wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu..
kauli ya serekali
serekali imewataka walimu wasigome na wanaowashawishi kugoma kwa kuwatumia msg waache.(taarifa hii imetolewa kwa hisani ya eafm)

DR ULIMBOKA APELEKWA NJE YA NCHI KWA MATIBABU ZAIDI

Kutokana na afya ya mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari kuendelea kuwa mbaya Jumuiya  ya madaktari  iliamua kumpeleka daktari huyo nje ya nchi ili aweze kupata matibabu zaidi kutokana na hospitali  umma  hapa nchi  kukosa vifaa muhimu ambavyo lati kama  vingekuwepo basi dokta asingepelekwa nje ya nchi.katika hatua nyingine hali ya utolewaji wa huduma imezidi kudhorota kupita kiasi kwenye hospitali za umma kutokana na mgomo wa madaktari kushika kasi na baadhi ya madaktari kufukuzwa kazi katika mikoa ya  mbeya,Mwanza na Kilimanjaro.
Serekali yatolewa nje
Katika hatua nyingine madaktari wamegoma kuchukua msaada wa serekali walioonyesha nia ya kutaka kumsaidia dr ulimboka gharama za matibabu nje ya nchi..wamesima wao kama madaktari na wadau wa afya pamoja na jamii imeshajipanga kusimamia matibabu ya dokta hivyo hawahitaji msaada kutoka serekalini.
Wananchi wasikitishwa
Wananchi mmoja ameaamua kuacha kuendesha pikipiki ambayo ndo iilikuwa biashara yake kwa kuhofia kuwa kama akipata ajali kipindi hiki cha mgomo basi angeshindwa kupata matibabu na kama ni kidonda kingeoza .wengine walisikika wakisema kuwa wanasiasa ndo wamewafikisha hapa kwa kuwa wanaleta siasa kwenye roho zao .Wakazidi kulaumu kuwa wamejiongezea posho wabunge na madiwani huku madaktari,wanafunzi,walimu  na wananchi  kwa ujumla wa kitaabika kwa matatizo mbali mbali ambayo yanaweza kutatuliwa kama wangeweka kipaumbele mambo ya muhimu kwanza.

snoop dog dog akamatwa na dawa za kulevya norway

rapper snoop amekamatwa na gram 8 za madawa ya kulevya(marijuana)  kwenye uwanja wa ndege wa Kjevic Airport in Kristiansand  huko norway.pia alikuwa na kiasi kikubwa cha pesa kuliko kile kinachoruhuhusiwa kusafiri nacho kwenye ndege..hii ni mara ya pili kwa rapa huyu kukamatwa na madawa ya kulevya ndani ya muda wa mwaka mmoja.

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara





Taarifa zilizotufikia zinadai kuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt. Fenella Mukangara amepata ajali ya gari wakati akielekea jijini Mwanza leo. Waziri Mukangara amepata ajali hiyo mkoani Tabora wakati akielekea jijini Mwanza kwa shughuli za wizara yake. Gari la Mukangara limegongana na basi la Green Star na waziri huyo amelazwa kwa matibabu. Taarifa zaidi zitawajia baadae.kwa hisani ya global publisher

SHUKRANI KUTOKA SK-NETWORK

SK-NETWORK ni mtandao bora na wa kisasa unaomilikiwa na vipeperushi company .kampuni inayohusika na utoaji na usambazaji wa vijarida vya matangazo nchini Tanzania inawatangazia umma wa watanzania kuwa wako katika hatua za mwisho za kubora huduma zao za matangazo ya hewani na nchi kavu(usambazaji wa vijarida)kuwa ya kisasa na kuwafikia watanzania milioni 1 ndani na nje ya nchi yetu.Hivyo basi tunafuraha kubwa kuwataarifu watazamaji wa blog zetu  kuwa tunaendelea kukuwa na kwa sasa tunatazamwa na watu wengi kutoka ndani na nje ya mpaka yetu.Tunakushukuru wewe mtazamaji wetu kwa kuchukuwa muda wako kuwaambia  jamaa,ndugu,marafiki nawapendwa wako kuhusu mtandao wetu  na jinsi ya kuupata ili nao waweze kupata habari na kuhabarika kwa haraka.Ili adhima yetu iweze kutimia ya kuwafikiwa watanzania milioni 1kwa siku. Tunakuomba uendelee kuwataafifu na jamaa wengine ambao kwa namna moja au nyingine hawajafikiwa na taarifa kuhusu SK-NEWORK.
Kumbuka kwa sasa SK-NETWORK inatoa ofa ya kutangaza bure kwenye blog yake ya masokoni.blogspot.com.changamkia fursa hii sasa kabla ofa haijaisha.

waziri mwinyi awatishia madaktari



waziri wa afya amewaambia madaktari watakoendelea na mgomo wao watakuwa wameikiuka mahakama iliyoamrisha kusitisha mgomo wa madaktari...onyo hili limetoka baada ya madaktari kuanza ngomo wao kuanzia jana jumapili katika hospitali mbalimbali za umma hapa nchi....hi si mara ya kwanza kwa madaktari kuamuua kugoma  wakishinikiza serekali iwaongezee mshahara na mahitaji mengine pamoja na kuboresha mazingira yao ya kazi..na mengine mengi kama kupatiwa nyumba za kuishi maeneo yakaribu na vituo vyao vya kazi..

michael essien na nadia buari wakikiss ..

jamaaa anakaribishwa home hivyo na mtotooo..chezeaaa ustar raha mida mingineee

mapesa ya safari za JK yatoweka

SERIKALI imeanza uchunguzi wenye lengo la kubaini kama maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walifuata taratibu kutoa  Hazina Sh3.5 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya safari za Rais Jakaya Kikwete ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa, Bernard Membe alisema jana kuwa fedha zinazochunguzwa ni zile zilitolewa kati ya Machi Mosi na Machi 8, mwaka huu kwa ajili ya safari za Rais Kikwete kwenda Geneva, Brazil, Adis Ababa na Arusha.

Wiki iliyopita gazeti moja la kila wiki liliripoti kuwa maofisa watano wa wizara hiyo wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuiba fedha zilizotengwa kwa ajili ya safari za rais kutoka benki moja nchini.

Fedha zilizotolewa kutoka Hazina ni Sh 3.5 bilioni wakati zilizokuwa zimepangwa kwa safari hizo ni Sh2 bilioni.Fedha hizo zinadaiwa kutolewa Hazina na maofisa waliokuwa wakikaimu nafasi mbalimbali, katika wizara hiyo.

Waziri Membe alisema wakati tukio hilo likitokea, yeye, naibu wake, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na Mhasibu Mkuu walikuwa safarini na kwamba nafasi zao zilikuwa zinakaimiwa.“Waliokuwa wanakaimu wali-process (andaa) fedha za safari pamoja na hazina, na fedha zikapatikana tarehe 8,” alisema Membe na kuongeza kuwa;

“Ofisa Masuhuri hakushirikishwa na uchunguzi wa kamati unaendelea ili kujiridhisha kama taratibu zote za kiutawala zilifuatwa,” alisema.

Alifafanua kwamba tayari walifanya uchunguzi uliohusisha Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Usalama wa Taifa na wakaguzi wawili kutoka wizarani hapo.“Hakuna tuliyemshuku ama kumuita mwizi kwa sababu hakuna hata fedha iliyoibwa, zote ziliingia kwenye akaunti ya wizara na nyingine zililetwa wizarani,” alisema.

Waziri huyo alisema uchunguzi wa kamati unaoendelea, sasa unalenga kuangalia kama taratibu zilifuatwa na wale waliokuwa wanakaimu.“Uchunguzi wa kamati utakapokamilika na kubainika makosa yalikuwa wapi utawekwa hadharani,” aliahidi.
Utabiri wake Chadema

Akizungumzia taarifa za kuitabiria Chadema ushindi mwaka 2015, Membe aliwatuhumu watu aliowaita maadui wake kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), akisema wameshiriki kumlisha maneno ya kukitabaria ushindi chama hicho kikuu cha upinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

"Kuna taarifa za mimi kutabiria ushindi Chadema 2015. Naomba niseme kitu kimoja, kama kuna mtu anajua mimi niliwahi kufanya utabiri ajitokeze. Mimi siyo TB Joshua wa Nigeria, mtoto wa marehemu Shehe Yahaya au (jina la kampuni moja ya kimataifa)...ambao wao kila mara ndiyo hufanya utabiri," alisema Membe huku akionekana kuchukizwa na taarifa hizo.

Membe alifafanua kwamba, ni kweli alikutana na ujumbe wa Chadema nyumbani kwake jimbo la Mtama, mkoani Lindi na kufanya nao mazungumzo, lakini hakuwahi kutabiri kwamba chama hicho kikuu cha upinzani kingeweza kushinda mwaka 2015.

"Nikweli nilifanya mazungumzo na Chadema walipokuja jimboni kwangu Mtama. Tena walikuja bahati nzuri walikuta chakula cha mchana tayari, nikawakaribisha vizuri. Wapinzani si maadui, yaani watu walitaka niwafukuze chakula. Najua kuna watu hawakufurahia kuwaalika Chadema kuja kwangu," alisema Membe na kuongeza;

"Ni kweli niliongea nao. Niliongea nao mambo matatu, kwanza niliwapongeza kwa kujipenyeza hadi vijijini. Niliwaambia, ni vema mmetambua umuhimu wa kufika hadi vijijini maana mwaka 2010 mlilalamika kuibiwa kura wakati vijijini mlikuwa hamjafika. Lakini pia, nikawambia ni vema wametambua umuhimu wa kuanza kufanya siasa kwa kujenga hoja na tatu, nikawambia nyie fikeni vijijini sisi kina Membe hatujaanza kutimua vumbi."

Alifafanua kwamba, anaamini watu wa Chadema waliokuwapo katika mkutano huo ambao ni pamoja na Dk Slaa na Lema hawawezi kuzusha taarifa hizo zilizotolewa na kuongeza, "Nimesoma vizuri Political Science, adui wa kisiasa katika chama siku zote yumo ndani ya chama hicho. Kwa hiyo hata hili naamini limetoka kwa baadhi ya maadui ndani ya CCM na kwa Chadema ni maadui wa Chadema."  

Kuhusu APRM

Katika hatua nyingine, Membe alisema taarifa ya Tanzania kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kujitathmini wa Umoja wa Afrika (APRM), itajadiliwa mwakani nchini Addis Ababa.

Licha ya waziri huyo kukiri kwamba Tanzania inadaiwa dola za Marekani 800,000 za ada, alisema hiyo si sababu ya taarifa ya Tanzania kutojadiliwa mwaka huu kama ilivyotarajiwa.

Rais Kikwete alitarajiwa kuwasilisha ripoti ya Tanzania kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU), utakaofanyika Lilongwe, Malawi Julai 10 mwaka huu, lakini haitafanyika hivyo.
Wiki iliyopita gazeti hili liliripoti kuwa Rais Kikwete amezuiwa kuwasilisha taarifa ya Tanzania kutokana na deni hilo.

“Walitakiwa wajadili taarifa ile halafu walete maswali tujibu ndipo wataandaa taarifa ikajadiliwe,” alisema Membe na kuongeza;

“Watu wa APRM hawajaja, hivyo itajadiliwa katika mkutano wa Addis Ababa mwaka 2013,” alisema.
Tanzania inadaiwa dola za Marekani 800,000  deni ambalo ni malimbikizo ya ada ya dola 100,000 kila mwaka, kwa miaka minane mfululilizo tangu mwaka 2005.

“Mara kwa mara tumekuwa tukiwakumbusha Hazina kuhusu deni hili na si kwamba ndilo limezuia,” alisema. 






habari ni kwa hisani ya gazeti la mwananchi.

break newz:::msanii ndani ya jeneza


umaarufu kuupata inahitaji ubunifu na kujitoaa muone sasa huyu jamaa toka nigeria alipoamua kuvunja rekodi kwa kuweka pozi kali ndani ya jeneza....stori yote hapo chini....
Controversial - , who is a grown man but still retaining the name that carries BOY, was said to have taken this particular picture showing him in a cofin all by himself. If another celebrity had taken such a picture and posted it, Nigerians would have made so much noise about such an abnormal occurrence, but since it is the man known for ‘out of space’ actions, most Nigerians just laughed over it and said ‘IT’S ’. What kind of man does that?

next step our website.....soon,,

sokoni kariakoo

vita vya drake na cris brown




drake akana kushiriki vurugo hizo
Following news that Drake and Chris Brown clashed last night at W.i.P. in New York City, New York, the Young Money rapper has denied responsibility for the cut on the singer's face.
In a statement released to TMZ, Drake's rep said that he had nothing to do with the brawl. Drake did not participate in any wrongdoing of any kind last night at W.i.P. He was on his way out of the club when the altercation began," said the rep. "[Drake] did not engage in any activity which resulted in injury to person or damage to property.”
Reportedly, Meek Mill was shouting at Brown, which incited the fight. The subject of the argument was reportedly not about Rihanna.
 tutaendelea kukupa taarifa kuhusu hili sakata lililopelekea cris kuchanika kidevu ...

je tutakuja kuwa na vitu kama hivii kweli???

 hii ndo jengo refu kuliko yote duniaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
hiki kitu kimajengwa huko dubai..barabara ya mbiguni hiyooo....
m naona kama inawezeka vile Tanzania  tukaja kuwa na vitu kama hivi ingawa itachukua sana  muda kwa kuwa kwa sasa wengi wetu ni wanafiki na tunapenda kuwa kama vinyonga vile kwenye ukweli unaweka na uongo ili upate pesa mbuzi ya mchelee...tukibadilika na kuwa watu makini si waongo na wanafiki basi maendeleo kama haya hayata kuwa ndoto kwetu kabisaaa.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...