.

Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts

break news:NAKALA YA MWISHO YA MWANAHALISI HII HAPA


nakala ya mwisho ya tovuti ya mwanahalisi hii hapaa....... icheki..
www.mwanahalisi.co.tz

gazeti la mwanahalisi limefungiwa kwa muda usiojulikana 
kuanzia tarehe 30/7/2012 

WALIMU TANZANIA WAANZA KUGOMA RASMI KUANZIA LEO


taarifa rasm kutoka kwa viongozi wa chama cha walimu tanzania zinasema  kuwa mgomo wao usio na kikomo unaanza leo rasmi  kutokana na kushindwa kufikia muafaka kati yao na muajiri wao ambaye ni serekali.walisisitiza kuwa mgomo wao hauto adhiri  sensa inayotarijiwa kufanyika tarehe 26 na kushirikisha kwa kiasi kikubwa walimu kama wadodosaji.

fwatilia kitabu hichi ndani ya maktaba yetu

www.makatabayetu.blogspot.com hii ndo maktaba ya sk network inayotoa nakala za kilele cha ubepari na tishio la ushoga...
hiki ni moja ya kipande cha kitabu hicho....karibu...


Nini tufanye?
Kwa haraka cha kufanya ni kuunda umoja na kudai mabadiliko ya dhati.
Kufufua azimio la arusha kwa nguvu zote.
Kufilisi wale wote waliotuibia rasilimali zetu na kuwafunga jela.
Kuunda mikataba mipya kwa wawekezaji wote nchi.
Je utajiuliza tutawezaje vyote hivi jibu ni rahisi tu, Umoja ni nguvu tukiwa wamoja tutaunda taifa jipya na lenye mavuno bora zaidi(katiba mpya)

Afrika

Katika kipindi chote hiki tunapo shuhudia mabadiliko makubwa katika bara la afrika ni kwa sababu ya kuchoka kwa wananchi ugandamizwaji unaofanywa na walowezi na waafrika wenzetu wasio na nia njema wanakula keki ya taifa wachache na kutuacha maelfu tukifa kwa utapiamlo.
Makundi ya wanyonge walalamika na kudai mabadiliko ya dhati kutoka kwa viongozi wao lakini yalishindikana kwa kuwa ubinafsi hujengwa na roho na ni ngumu sana kubadilisha roho ya mtu.
Ardhi ya babu na bibi yangu Africa ilishuhudia damu ikimwagika mnyonge akipigwa bom na ili afe.ubinafsi huondoa uti ubepari haudhani roho ya myonge.
Mabepari wakauwa ndugu zetu wakawachimbia chini na kuwazika.lakini wachache waliobaki walipata nguvu pindi walipokuwa wanaenda mazishini kuzika wenzao na wakaamua wafie nchi kwao.
Mungu awalaze mahala pema peponi wanyonge wote waliofia mataifa yao wakipinga ubepari.

sakata la mafao

sakata la mafao la zua bala mpaka bungeni baada ya wabunge kuomba muuongozo sasa m najiuliza kama ilipitishwa na bunge sasa leo mbona wanaomba muongozo au kipindi unapita wabunge hawakuuelewa ..walisema tu ndio bila kujua kilichomo ndani...

chezea toyooo


nigeria ni nomaaa bongo mkijaribu hii lazima itawatokea puwaniii

Utafiti mpya uliofanywa sehemu mbali mbali za dunia, kutaka kujua wapi watu wanaficha fedha zao kukimbia kodi, umegundua kuwa dola kama trilioni 20, zimefichwa nchi za ng'ambo, mbali ya macho ya maafisa wanaotoza kodi.

Ripoti hiyo imeandikwa na shirika la utetezi, Tax Justice Network, ambayo inasema kuwa tofauti baina ya matajiri na maskini ni kubwa kuliko ilivofikiriwa.
Dola trilioni 21 ni sawa na pato la mwaka la Marekani nzima pamoja na Japani.
Tax Justice Network inafikiri fedha zilizofichwa ng'ambo zinaweza kuwa zaidi ya hizo.
Ripoti yao inaonesha jinsi matajiri wakubwa wanavohamisha fedha na kuziweka kwenye nchi zinazoweka siri, kama Uswiswi na Visiwa vya Cayman, kwa kupitia mabenki ya kibinafsi.
Ripoti piya inaeleza kuwa nchi zenye utajiri wa mafuta, kama Urusi na Nigeria, ndio hasa kwenye mtindo wa fedha kutoweka na kuvushwa, badala ya kuwekezwa nchini.
Utafiti huo unamaliza kwa kusema wanasiasa sehemu mbalimbali za dunia, wanategemea kuwa fedha hata zikiwa kwa watu wa juu, zitavuja hatimae na kuwafikia maskini - ripoti inasema hayo hayatokei tena. kwa hisani ya bbc

MSANII Juakali kaokoa ndege isilipuke london


JUAKALI MSANII KUTOKA KENYA ALIJIKUPA AKIPATA BONUS 10 YA KUSAFIRI FIRST CLASS BAADA YA KUWASHITUA WAHUDUMU WA NDEGE WALIYOKUWA WAMEIPANDA BAADA YA KUONA INGINE MOJA YA NDEGE HIYO IKITOA MOSHI MWEUSI.SHIRIKA LA NDEGE LIMEMSHUKURU SANA MGENGE JUAKALI NA KUMUONGEZEA  ZAWADI KWA KUMLIPIA NAULI KWENDA   AMSTERDAM  LONDON.

WATU 14 WAFAA NA 50 WAJERUHIWA


Watu wapatao 14 wamefariki dunia na wengine 50 wamejeruhiwa cinema complex huko suburb,aurora,baada ya kijana aliyekuwa amevaa mask kuwapiga watu RISASI walikuwa wakifwatilia show ya the dark knight rises..pande za U.S.A

RAMADHANI NJEMA


SK NETWORK  UNAWATAKIA MFUNGO MWEMA WAISLAMU WOTE DUNIANI.

TAARIFA KWA UMMA


SK NETWORK INATOA POLE KWA WAFIWA WOTE NA WATANZANIA WOTE KWA AJALI MBAYA YA MELI ILIYOTOKEA JANA.MUNGU AWALAZE MAHALA PEMA PEPONI MAREHEMU WOTE.

ajali ya meli zanzibar



picha kutoka kwa wadau wa facebook zikionyesha maiti ambazo tayari zimeshapatikana na pia wahanga wakisubiri kuokolewa na boti za uwokozi wakiwa wamesimama na kukaa juu ya meli hiyo iliyo anza kuzama majira ya saba siku ya jana.


MELI YAZANA ZANZIBAR


Waokowaji wamefika eneo la tukio

Mv Karama ikiwa abiria 200 tayari juhudi za kuwaokowa wahanga wa meli hiyo zimeanza na tayari mamlaka husika zimeanza kuchukuwa hatuwa za kuwaokowa ikishirikiana na kampuni mbali mbali za usafiri wa baharini.

Muandishi wa ITV Farouk Karim akiwa katika eneo la tukio ameeleza kuwa ameona life jacket zikieleya majini zikiwa hazina watu na baadhi ya vifaa, na mtu mmoja ameokolewa akiwa hai.

NBS WATANGAZA NAFASI ZA KAZI...


Tangazo La Kazi Ya Muda Katika Mradi Wa Sensa Ya Watu Na Makazi Ya Mwaka 2012

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inakamilisha maandalizi ya kufanya Sensa ya Watu na Makazi ambayo itafanyika tarehe 26 Agosti, 2012. Ili kufanikisha Sensa hii, Serikali inatangaza nafasi za kazi za muda za MAKARANI NA MAKARANI WAANDAMIZI WA SENSA kwa Watanzania wenye nia na sifa zinazostahili kama ilivyoainishwa katika tangazo hili. Kazi hii itaanza tarehe 06 Agosti, 2012 na kumalizika tarehe 14 Septemba 2012.


tembelea www.nbs.go.tz

Peter mutharika kaka wa Bingu wa mutharika kugombea uraisi malawi 2014

baada ya Bingu wa mutharika kufa na urais wa nchi ya malawi kuchukuliwa na mwana mama ambaye alikuwa makamu wa rais kipindi cha uhai wa bingu sasa kaka mtu kasema ana nia sabiti ya kugombania urahisi mwaka 2014 kwa tiketi ya chama cha DPP na kwa hakika anaapa kuwa ni lazima chama chake kitachukua ushindi na kuingia ikulu ili akamalizie na kuendeleza yale aliyoyacha mdogo wake.

TANGAZO KWA UMMA

Karibu SK NETWORK
SK NETWORK ni moja ya mtandao mkubwa na maarufu  hapa nchini Tanzania unaojihusisha na utoaji wa huduma za promotion mitandaoni ikiwa na uzoefu wa miaka mitatu.
Sasa kuanzia tarehe (05/07/2012) tunatoa ofa ya kutangaza matangazo mawili ya biashara yako bure ndani ya mtandao wetu kila mwenzi.
Vigezo
1.       Video:Lazima liwe kwenye youtube kwanza.
2.       Picha:Picha zisizidi tatu.
3.       Words:isizidi kurasa moja (1)

K.K: SK NETWORK haina muda wa kurekebisha kazi yako hivyo basi isome zaidi ya mara moja kabla hujatutumia.
Tembelea blog zetu Kila Siku:
·         www.tanzaniamenu.blogspot.com
·         www.masokoni.blogspot.com
·         www.totolabongo.blogspot.com
·         www.maktabayetu.blogspot.com

          KAULI MBIO YETU: ((TUNATANGAZA, UNAUZA))
Itume hii taarifa hii kwa mtu yeyote mwenye  Biashara.


Wasiliana nasi: +255 713592224, +255767592224
 Barua pepe:sknetwork@live.com,sokonikariakoo@gmail.com

ASANTE.

afya ya DK ULIMBOKA yaanza kutengamaa



taarifa kutoka kwa wanaosimamia matibabu ya dr Ulimboka wanasema kuwa kwa sasa afya yake imeanza kutengamaa kidogo kidogo na inatia faraja hivyo basi watazania wezangu mzidi kumuombea DK ili azidi kupata nafuu na hatimae apone kabisa...

saba saba jengo la BUNGE



Je unajua ni lazima uombe kibali ili uweze kuingia bungeni na sendo kama wewe ni mbunge??je unajua ni maspika  wangapi waliokisha pita mpaka sasa.haya yote utayapata ndani ya jengo la bunge saba saba fanya hima nenda pale kesho ..kuna vingi vizuri na vya kuvutia.

CHINA WAITEKA SABA SABA

 MAONYESHO YA 36 YA SABA SABA......



KIJANA CHUI HUYO......
leo mdau ya SK NETWORK  ilikuwa  saba saba akifwatilia mambo ya fulani fulani katika banda moja wapo maeneo hayo..katika ripoti yake mdau wetu amekiri kuwa sabasaba ya sasa imekuwa na bidhaa nyingi sana za kutoka china .mpaka bidhaa zili ambazo tumezoea kuziona kwa wajasiliamali wa kawaida kabisa kutoka sido na wachina pia wanazo..ingawa si vibaya lakini kwa maono yake na wadau wachache waliohojiwa wamekiri kuwa china inanguvu kubwa ya matangazo na wanaummoja kutuzidi watanzania kiasi kwamba wanapata watazamaji wengi kuliko hata mabanda mengine ya bidhaa za aina kama yao...mabanda ya watanzania sasa  wengi wao  wamekutwa wakiwa wemenyongonyea na wengine hawakaribishi hata wateja..na pia mpangilio wa bidhaa zao hauvutie mteja kuangalia mara mbili... kama kweli tunahitaji kuwa  kwenye ushindani wa biashara na mataifa mengine kama Kenya na China ...basi inabidi tubadilike tuache kuweka vinyago na makatuni mlangoni wakichekesha wateja,,,bali tujitahidi kuweka bidhaa ,mabango ya kuvutia na  wahudumu wachangamfu.Benki fulani fulani zimechukua vijana na kuwaweka barabaran kuhamasisha wateja  jambo hilo si baya bali vijana hao muda mwengine wanageuka usumbufu pale unapokubali kuzungumza nao....Tembeleeni saba saba ya mwaka huu na uje na maoni yako na sisi tutayaweka hewani...











katuni


Serikali yaomba madaktari nje ya nchi(billioni 600 zatengwa kuwalipa)

((kwa hisani ya tanzania daima)
SERIKALI imeamua kuagiza madaktari kutoka nchi za nje watakaochukua nafasi ya wale wa hapa nchini ambao wamegoma kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita.
Habari kutoka katika moja ya vyanzo vya kuaminika zimesema kuwa uamuzi huo wa serikali ulipitishwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri kilichokutana mjini Dodoma juzi chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilidai kuwa Rais Kikwete alikerwa na tabia ya madaktari kupingana na serikali licha ya juhudi zote zilizofanywa kuboresha maslahi yao.
Kwa mujibu wa habari hizo, kiasi cha sh bilioni 200 kimetengwa kwa ajili ya kuwaleta na kuwagharimia  madaktari hao wa nje na pia baraza limepitisha azimio la kuzungumza na hospitali za jeshi kama  Lugalo na zingine ndogo kubeba jukumu hilo kwa sasa pamoja kuagiza madaktari wastaafu wote warejee kazini katika kipindi hiki cha mgomo.
Habari zimedai kuwa madaktari hao wanasadikiwa watatoka katika nchi rafiki, zikiwemo India, China, Cuba na Afrika Kusini, na kwamba wataziba kikamilifu pengo la wale wa hapa nchini ambao wamegoma.
Inaelezwa kuwa mara baada aya kukamilika na kuanza rasmi kwa huduma za matibabu, madaktari wa hapa nchini waliomo katika mgomo na wale zaidi ya 200 waliodaiwa kufukuzwa na serikali kimyakimya, watalazimika kurejeshwa kazini kwa masharti makali.
Hata hivyo, uamuzi wa serikali  kuwatimua madaktari wakati suala lao liko mahakamani, umewagawa wabunge.
Baadhi ya wabunge walijaribu kuhoji suala hilo Bungeni, lakini walikwama baada ya Spika Anna Makinda  kuzuia mjadala huo kwa madai kuwa suala hilo liko mahakamani.
Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangala, alisema kuwa kilichofanywa na serikali ni kiini macho kwani juzi Waziri Mkuu Mizengo Pinda  alisema serikali  haiwezi kutoa kauli dhidi ya madaktari kwa madai kuwa kuna kesi mahakamani.
“Juzi serikali imesema kuwa haiwezi kutoa kauli kwa vile jambo hilo lipo mahakamani, sasa imewezaje kuwafukuza madaktari wakati jambo lipo mahakamani?” alihoji Dk. Kigwang’ala.
Aliitaka serikali kuondoa kesi hiyo ili kurejesha majadiliano kwani ndio njia pekee ya kukabiliana na mgogoro huo.
Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, alimshangaa Spika Anna Makinda kuzuia mjadala huo kwani ungeweza kujadiliwa bila kuingilia uhuru wa mahakama.
Juzi uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,  uliwafukuza kazi madaktari 229 walioko katika mafunzo kwa njia ya vitendo kutokana na mgomo unaoendelea wa kushinikiza  kulipwa posho zao za mwezi mmoja.
Hospitali zingine ambako madaktari wamefukuzwa kutokana na mgomo huo ni pamoja na Mbeya na Dodoma.
Jeshi lachukua nafasi za madaktari
Wakati huo huo Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limeanza kutekeleza kwa vitendo agizo la serikali la kutoa huduma za kitabibu kwa wagonjwa kufuatia mgomo wa madaktari nchini.
Juzi Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwa bungeni alisema serikali imeamua kuwatumia madaktari waliopo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wastaafu na hospitali zote za jeshi kuendelea kutoa huduma ya matibabu kwa wagonjwa.
Msemaji wa JWTZ Kanali Kapambala Mgawe katika mahojiano maalum na gazeti hili, alisema juzi baada ya Waziri Mkuu Pinda kutoa agizo hilo, walianza utekelezaji wake ambapo kwa jiji la Dar es Salaam, hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Kikosi ya 521, Mgulani na ile ya Kikosi cha Navy-Kigamboni na hospitali zake zote kote nchini zilianza kutoa huduma hiyo bila vikwazo.
“Kwanza naomba umma uelewe hivi hospitali za JWTZ hapa nchini kwa asilimia 70 zimekuwa zikiwatibu raia bila vikwazo vyovyote hivyo agizo hilo la serikali huenda likaongeza idadi ya wagonjwa kutibiwa katika hospitali zetu labda kwa asilimia 90.
Mgawe alisema madaktari wanajeshi wapo kwa ajili ya kulinda taifa na watu wake, hivyo akawahakikishia wananchi wanaougua kutosita kwenda katika hospitali za jeshi hilo kutibiwa akidai kuwa hawaoni mantiki ya daktari kugoma.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...