.

Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

mnyika kafafanuaaa kauli zakee

Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.
Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais anamamlaka ya kumuamrisha waziri wa fedha aiondowe bajeti……kwa hisani ya global publisher.



mapesa ya safari za JK yatoweka

SERIKALI imeanza uchunguzi wenye lengo la kubaini kama maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walifuata taratibu kutoa  Hazina Sh3.5 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya safari za Rais Jakaya Kikwete ndani na nje ya nchi.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa, Bernard Membe alisema jana kuwa fedha zinazochunguzwa ni zile zilitolewa kati ya Machi Mosi na Machi 8, mwaka huu kwa ajili ya safari za Rais Kikwete kwenda Geneva, Brazil, Adis Ababa na Arusha.

Wiki iliyopita gazeti moja la kila wiki liliripoti kuwa maofisa watano wa wizara hiyo wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuiba fedha zilizotengwa kwa ajili ya safari za rais kutoka benki moja nchini.

Fedha zilizotolewa kutoka Hazina ni Sh 3.5 bilioni wakati zilizokuwa zimepangwa kwa safari hizo ni Sh2 bilioni.Fedha hizo zinadaiwa kutolewa Hazina na maofisa waliokuwa wakikaimu nafasi mbalimbali, katika wizara hiyo.

Waziri Membe alisema wakati tukio hilo likitokea, yeye, naibu wake, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na Mhasibu Mkuu walikuwa safarini na kwamba nafasi zao zilikuwa zinakaimiwa.“Waliokuwa wanakaimu wali-process (andaa) fedha za safari pamoja na hazina, na fedha zikapatikana tarehe 8,” alisema Membe na kuongeza kuwa;

“Ofisa Masuhuri hakushirikishwa na uchunguzi wa kamati unaendelea ili kujiridhisha kama taratibu zote za kiutawala zilifuatwa,” alisema.

Alifafanua kwamba tayari walifanya uchunguzi uliohusisha Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Usalama wa Taifa na wakaguzi wawili kutoka wizarani hapo.“Hakuna tuliyemshuku ama kumuita mwizi kwa sababu hakuna hata fedha iliyoibwa, zote ziliingia kwenye akaunti ya wizara na nyingine zililetwa wizarani,” alisema.

Waziri huyo alisema uchunguzi wa kamati unaoendelea, sasa unalenga kuangalia kama taratibu zilifuatwa na wale waliokuwa wanakaimu.“Uchunguzi wa kamati utakapokamilika na kubainika makosa yalikuwa wapi utawekwa hadharani,” aliahidi.
Utabiri wake Chadema

Akizungumzia taarifa za kuitabiria Chadema ushindi mwaka 2015, Membe aliwatuhumu watu aliowaita maadui wake kisiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), akisema wameshiriki kumlisha maneno ya kukitabaria ushindi chama hicho kikuu cha upinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

"Kuna taarifa za mimi kutabiria ushindi Chadema 2015. Naomba niseme kitu kimoja, kama kuna mtu anajua mimi niliwahi kufanya utabiri ajitokeze. Mimi siyo TB Joshua wa Nigeria, mtoto wa marehemu Shehe Yahaya au (jina la kampuni moja ya kimataifa)...ambao wao kila mara ndiyo hufanya utabiri," alisema Membe huku akionekana kuchukizwa na taarifa hizo.

Membe alifafanua kwamba, ni kweli alikutana na ujumbe wa Chadema nyumbani kwake jimbo la Mtama, mkoani Lindi na kufanya nao mazungumzo, lakini hakuwahi kutabiri kwamba chama hicho kikuu cha upinzani kingeweza kushinda mwaka 2015.

"Nikweli nilifanya mazungumzo na Chadema walipokuja jimboni kwangu Mtama. Tena walikuja bahati nzuri walikuta chakula cha mchana tayari, nikawakaribisha vizuri. Wapinzani si maadui, yaani watu walitaka niwafukuze chakula. Najua kuna watu hawakufurahia kuwaalika Chadema kuja kwangu," alisema Membe na kuongeza;

"Ni kweli niliongea nao. Niliongea nao mambo matatu, kwanza niliwapongeza kwa kujipenyeza hadi vijijini. Niliwaambia, ni vema mmetambua umuhimu wa kufika hadi vijijini maana mwaka 2010 mlilalamika kuibiwa kura wakati vijijini mlikuwa hamjafika. Lakini pia, nikawambia ni vema wametambua umuhimu wa kuanza kufanya siasa kwa kujenga hoja na tatu, nikawambia nyie fikeni vijijini sisi kina Membe hatujaanza kutimua vumbi."

Alifafanua kwamba, anaamini watu wa Chadema waliokuwapo katika mkutano huo ambao ni pamoja na Dk Slaa na Lema hawawezi kuzusha taarifa hizo zilizotolewa na kuongeza, "Nimesoma vizuri Political Science, adui wa kisiasa katika chama siku zote yumo ndani ya chama hicho. Kwa hiyo hata hili naamini limetoka kwa baadhi ya maadui ndani ya CCM na kwa Chadema ni maadui wa Chadema."  

Kuhusu APRM

Katika hatua nyingine, Membe alisema taarifa ya Tanzania kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kujitathmini wa Umoja wa Afrika (APRM), itajadiliwa mwakani nchini Addis Ababa.

Licha ya waziri huyo kukiri kwamba Tanzania inadaiwa dola za Marekani 800,000 za ada, alisema hiyo si sababu ya taarifa ya Tanzania kutojadiliwa mwaka huu kama ilivyotarajiwa.

Rais Kikwete alitarajiwa kuwasilisha ripoti ya Tanzania kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU), utakaofanyika Lilongwe, Malawi Julai 10 mwaka huu, lakini haitafanyika hivyo.
Wiki iliyopita gazeti hili liliripoti kuwa Rais Kikwete amezuiwa kuwasilisha taarifa ya Tanzania kutokana na deni hilo.

“Walitakiwa wajadili taarifa ile halafu walete maswali tujibu ndipo wataandaa taarifa ikajadiliwe,” alisema Membe na kuongeza;

“Watu wa APRM hawajaja, hivyo itajadiliwa katika mkutano wa Addis Ababa mwaka 2013,” alisema.
Tanzania inadaiwa dola za Marekani 800,000  deni ambalo ni malimbikizo ya ada ya dola 100,000 kila mwaka, kwa miaka minane mfululilizo tangu mwaka 2005.

“Mara kwa mara tumekuwa tukiwakumbusha Hazina kuhusu deni hili na si kwamba ndilo limezuia,” alisema. 






habari ni kwa hisani ya gazeti la mwananchi.

nyie ssm na chadema nyieeeee ;;;;hayaaa

hii ndo yetu tanzaniaaaaaaa....nyie huku mnagangana na kuzozana na kuvaa na kuvaa gambaaa haya banaaaaaaaaaaaaaaaa........(picha kwa hisani ya UMASIKINI TANZANIA BLOG)..hawa ndo waasisi..sisi huku mjini tunafanya upuuzi tu na sifaa za kijinga wakati mamia wanatesaka kijijin...nyiee watu jiribuni hata kutumia akili za shingoni kama za kichwani hazipoooooooo.

nini dhambi kwa mwenye dhiki???

chadema na ccm mnajua mnao wawakilisha au mnapiga tu mbembe mbembe.....kitaa kina njaa sanaa wanasiasa acheni utani utani fanyeni kazi inayoonekana huko maji hakuna umeme bae na mgao unakujaa...hakuna kitu tunakomaa lakin hatufanikiwi.............hii ni vita mazeee tunakufa bila kujijiuaa  inabidi tuamike na tusake chapaa na tuokoe kitaaaaaa...eee Mungu utusaidieeee

kanisa lachomwa moto zanzibar

kanisa likiwa limeteketena na kuisha kabisaa huko zanzibar kanisa la TAG huko pande za zanzibar.

ujumbe wa leo kwa CCM NA CHADEMA

leo nilikuwa mitaa ya kiwalani minazi mrefu nikakutana na huu ujumbe katika ofisi ya mwenyekiti wa mtaa ningependa ni share na wadau wote wa blog yetu na hasa hawa wanachama wa ccm na chadema wajue ujumbe huu kwa makini .....ukiwa unafanya kitu kwa mfumo huu huji kufanikiwa milele..zingatia huuu ujumbee....kuwa makini kila dakika....michuzi michuzi ya leo ndo hiyoooo.......msg send.........ok

vua kanga vua kofia vaa gwanda(chadema &ccm)

kesho majira ya saa nane mchana kutakuwa na mkutano mkubwa wa chadema viwanja ya jangwani ukiwa ni mfululizo wa ile season ya kuvua kanga na kofia na kuvalisha gwanda na kuingia vitani...unaongeshwa pale jangwani kesho unapata ubatizo wa kisiasa............N.B nyie wanasiasawa sasa  kumbukeni huku kitaa hizo sera zenu bado hazijaa matunda ya moja kwa moja bado mateso ni makubwa sana kwetu sisi wananchi wa hali ya chini kweli tunateseka tunahitaji nguvu yenu muiweke kwenye vitu vya msingi sio vaa kanga vaa ngandwa pekee yake..hadi leo sukari bado juu,umeme juu,maji juu nyie mnagangana na vaa gwanda vua kanga ...

mbunge wa rombo apata ajali(Joseph Selasini)

Mbunge wa Rombo apata ajali mbaya iliyosababisha vifo vya watu watatu.Ajali hiyo imetokea kwenye eneo la bomang'ombe..

michuzi michuzi ya CCM NA CHADEMA


je hii kauli mbio ya vua gamba vaa gwanda ina maana gani?je ushawahi tafakari dhumuni kuu la wavua magamba na kukimbia gwanda...au ndo kama msemo wa siku hizi usemavyo unanuka  kaoge?hiyo kuoga kisiasa kwa hapa bongo ni kuvaa gamba ..fasta .au??? m bado natafakari ipo siku nitakuja na jibu...ila kwa sasa m  yangu machooooooooooooooooo..wanasiasa kumbukeni kila siku vitu vinapanda bei,, wakubwa ..tunakufa sisi watu wa hali ya chini...............tuoneeni huruma japo kidogo wakubwaa.

nani ataibuka mshindi 2015???

kwa hali ilivyo sasa umasikini unazidi kutuuua watu wa kima cha chini  na hili ndo jamga kubwa kuwahi kutokea  hapa  kwetu Tanzania...mfumuko mkubwa wa bei na changamoto ngumu tunazozipa wananchi pindi tunapohitaji huduma za kijamii..hasa afya na elimu mambo bado magumu kwa masikini wa taifa hili..na kwa kiasi kikubwa siasa imeonyesha kushindwa kutibu majanga haya zaidi ya kuyapuliza tu kwa muda mfupi..na baada maumivu huanza upya tena kwa kasi kubwaaaaa....nani atashinda 2015?...ni wewe au yule ..na kwa nini wewe na asiwe yule...jipime mapema..okoa taifa sasa ukisubiri 2015 utakuta taifa tupu...lisilo na watu..okoa taifa   sasa....okoa taifa sasa...iwe ni ccm ,cuf,chadema ,nccr n.k.................tambua kuwa leo ndo ipo tanzania kesho ni majaliwa ya Mola kuiona...okoa nchi yako leo...kuwa muadilifu sasa...chapa kazi sasa......timiza ahadi sasa...tuokoe watanzania sasa kwa kuwa mzalendo.....tembelea mara kwa mara uchaguzi2015.blogspot.com

misri vifo kila kukichaa

Watu wasiojulikana wamewaua waandamanaji 11 waliopiga kambi nje ya makao makuu ya Watawala wa Kijeshi Mjini Cairo,Misri.
Maafisa wanasema watu hao walianza kuwashambulia kwa mawe, mabomu na risasi waandamanaji hao ambao pia walijibu mashambulizi hayo. Wanajeshi pamoja na polisi wamezika makabiliano hayo, lakini baada ya saa sita za vurugu.

Abdul Moneim Aboul Fotouh,mgombea wa kujitegemea pamoja na kiongozi wa chama Freedom and Justice Party ambacho kinaungwa mkono na Muslim Brotherhood Mohammed Mursi wamelaani maafisa wa usalama kwa kuchelewa kuzuia fujo hizo.Kufuatia tukio hilo wagombea wawili wakuu wa Urais wamesimamisha kampeini zao kulalamikia mauaji hayo.
Aidha chama cha FJP na kile cha Salafist Nour ambavyo vina wabunge wengi vimesusia mkutano na Baraza tawala la kijeshi{Scaf}.
Maandamano kulalamikia utawala wa kijeshi yameendelea tangu jeshi lichukue madaraka baada ya kuondolewa kwa Rais Hosni Mubarak Februari mwaka 2011.
Watawala wa Kijeshi wamelaumiwa kwa kuwakandamiza wapinzani na kuwaua waandamanaji pamoja na kuzima mashirka ya kiraia.
Watawala wa kijeshi hata hivyo wameahidi kuyakabidhi madaraka kwa raia mwishoni mwa mwezi Juni baada ya kufanyika uchaguzi wa Urais ambao wanasema utakuwa huru na haki.

maajabu ya diwani wa kwala kuchinja ng'ombe mkutanoni..

maajabu ya diwani wa  kwala ni baada ya kuamua kuchinja ngombe na kuandaa wali wengi ili kuwavutia wananchi waje kwenye mkutano  wake wa hadhara alioufanya katika kata ya kwala tarehe 26/4/2012 ..diwani huyo wa tiket ya ccm hakujali adha wanaoipata wananchi wake kwa kukosa maji safi ya kunywa wa kipindi kirefu sasa ......
 
darasa la shule ya msingi kwala
ila yeye alitafuta pikipiki na kwenda kufwata maji huko mwaloni kwa ajili ya shughuli zima ya kupika wali na nyama kwa ajili ya mkutano wake huo.....


fanya zoezi hii???????
 maeeneo ya kwala ndipo anapopatikana muwekezaji wa kuku kunoga ambaye amesaidia sana kijiji cha kwala kupata maji safi na salama ya kunywa kwa kipindi cha nyuma kabla transforma halija haribika..kwa kipindi kirefu sasa transforma imeharibika na wanakijiji wa huku wanapata mateso makubwa kutafuta maji umbali mrefuuu.
mavazi ya wageni hayo hapo..
maoni ya wanachi yalikuwa yakitofautia sana kuhusu swala hili la diwan kupika wali wakati wao hawana maji wengi walisema kuwa elimu ndogo maeneo ya vijijin husababisha viongozi wetu wengi kujisahau na kufanya mambo kimazoeaaaaaa

VIJANA WAIKANA CCM(WABUNGE WATABIRI KIFO 2015)

 KUNDI KUBWA LAVIJANA KLAENDELEA KUKIHAMA CHAMA TAWALA CHA CCM NA KUJIUNGA NA CHAMA CHA UPINZANI CHA CHADEMA KWA KILE KINACHOSEMWA KUWA SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA..................WANAHAMA NA KUHAMISHIA MATUMAINI YAO KWA CHADEMA JE WATAPONA ...MAANA KUWA CHADEMA KUNAHITAJI UJASIRI MKUU...SI UNAONA MAMA HAPO JUU WALIVYOMFANYA ....JE NINI KITAENDELEA PINDI CHAMA TAWALA KITAPOKOSA NGUVU YA VIJANA...TAFAKARII NA CHUKUA HATUA..
...
picha hii  ni hisani ya wadau wa facebook
WANAJAMII WANAAMINI KUWA JENEZA LA CHAMA TAWALA LI NJIANI JE NI KWELI...?JE SIASA HIZI ZA KUHAMA VYAMA ZINA TIJA YOYOTE KWETU WANANCHI..?
MBUNGE WA MBOZI KWA TIKETI YA CCM AMEITABIRIA KIFO KISICHO NA WAOMBOLEZAJI CHAMA CHAKE CHA CCM KWA KUWA WANAWAACHA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI WAKILA HELA ZA UMMA NA MAKATIBU WA WIZARA WAKATI WANANCHI WAKILIA SHIDA HUKU MITAANI,,AKIKANA WAZI WAZI CHAMA CHAKE NA KUSEMA HATO SHANGAA PINDI WATAKAPO SHINDWA UCHAGUZI MKUU MWAKA 2015..NA HATA WAKISHINDA  MWAKA 2015 BASI 2020 HAWATONYOFOKA NI LAZIMA CCM ITABAKI HISTORIA KWA MADUDU WANAYOFANYA SASA....WAKURUGENZI WETU NA SEREKALI KWA UJUMLA .(KUTOKA DODOMA BUNGENI)
sokoni kariakoo

pole sana Lema

kweli hii ni nomaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa tupu.hiiiiiiiiiiiiiiii tanzania pole sana mr Lema na wananchi tunalipa kodi ili zijengwe barabara na miundo mbinu ila pesa zetu zinatumika kwa uchaguzi na kulisha watu wasio na kazi zozote zile za msingi sasa sawa mpaka 2015 hiki ni kipindi cha kufanya uchaguzi tuu..hakuna kingine kwa wale watakao ngatuliwa na pia watakao kufaa ...cost zote hizo zipo chini yetu wananchi..walipa kodi wa tanzania..
sokoni kariakoo

pipozzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz


naona chadema wanawekeza maisha na vijana wenye umri mdogo .....inamaanisha kama ni club ya mpira basi chadema ni zaidi ya asnal au barca....hongereni kwa ushindi    pia ccm ongereni kwa kukubali kushindwa...maana asiyekubali kushindwa si mshindani...maisha yanaendeleaaa..............peoplesssssssssssssssss power .........na wana wa hapo vipi...............hapo poaa..
ulikuwa mpambano mkalliiiiiii sana wa kihistoriaaa.
sokoni kariakoo

Tunatangaza mgao rasmi,,,huu wa nyuma ni rasha rasha tu..

kama vile wananchi wanavyokuwa wakisubiria mvua za vuli na masika ndivyo hiyo hiyo watanzania huwa wakisubiria umeme kuwaka au kukatika...ingawa walipandisha kiwango cha tozo bado mgao wa utaendelea kama kawaida...mimi kwa mawazo yangu  naona tunacheza na masikini wa nchii hii..hawana maji ,hawana umeme,hawana ajira kweli hii nchi si itakuwa jehanamu yao jamani..ukweli unafichwa fichwa kwa sisi wanyonge hatujui APTL ndo nini na hao AGGRECO  juzi tu niliona wanashusha makontena pale ubungo tena chini ya gred ya taifa wakaweka majenereta yao leo wameshaanza kuzingua tenaaa.. Mwananchi tuachane na mambo ya Arumeru tulijadili taifa letu...ges sasa inauzwa 60000 toka 32000 miezi kadhaa iliyopita ...misosi usigure kilo ya mchele 3000..kweli kunakutoka hapa kweli...mungu bariki nchi yetu ya Tanzania.haya sasa washatangaza mgao rasmi na sisi tumeshakubali kukaa giza ila tanesco mjue mlituomba miezi sita ya nyongeza ya bili ikipita hiyo turudishieni tozo za mwanzo...

ADC NA CHADEMA BENDERA ZAO SASA..



wapinzani wazidi kuchukua madaraka katika nchi zetu za afrika(hongera senegal) na kuendelea kuwa na wabunge wengi kuliko miaka ya nyumaa..kutokana na hilo basi vyama vingi vimezuka na kuchukua usajili..ingawa sasa kunaukosefu mkubwa wa umakini kwa mfano bendera ya chadema na chama kipya cha ADC zinafanana..hii inamaanisha nini au ndo kimewekwa ili kudanganya wananchi ....hii ndo siasa ya afrika...vyama kwa wingi sio vyama vingi tenaaa.

wakimbizi wakimbia huku na kule...mali


wakimbizi toka mali wakiwa kijiji cha chinagodrar ,tillabery region,Niger wakikimbia mapigano yanayoendelea nchi mwaoooo...UN yaomba msaada wa chakula na kuomba nchi za jirani zijiandae kupokea wakimbizi wengine  wengi toka mali kuazia sasa.......(ingawa kwao kukame ila maji yapo Tanzania kimara tu maji shida sasa huko singida inakuwajeeee?????tafakariiiiii???)
sokoni kariakoo

kikosi cha mali kilichochukua nchi...vijana wadogoooo

hawa ndo baadhi ya timu ya vijana wa mali walioamua kuchukua nchi..kwa mapinduzi ya fasta fasta kwa kupiga uwepo wa wavamizi katika nchi yao huku serekali iliyopo madarakani ikiwa haichukulii swala hilo kwa uzito..sasa wanachokifanya ni kuhakikisha wanalinda mipaka yote ya nchi ...na kuandaaa uchaguzi wa kidemkrasia  .....vijana hao je wazo lao litafanikiwa kweli maana shinikizo lashaaza toka kwa hawa wanaojiita umoja wa mataifaa...
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...