Ripoti hiyo imeandikwa na shirika la utetezi, Tax Justice Network, ambayo inasema kuwa tofauti baina ya matajiri na maskini ni kubwa kuliko ilivofikiriwa.
Dola trilioni 21 ni sawa na pato la mwaka la Marekani nzima pamoja na Japani.
Tax Justice Network inafikiri fedha zilizofichwa ng'ambo zinaweza kuwa zaidi ya hizo.
Ripoti yao inaonesha jinsi matajiri wakubwa wanavohamisha fedha na kuziweka kwenye nchi zinazoweka siri, kama Uswiswi na Visiwa vya Cayman, kwa kupitia mabenki ya kibinafsi.
Ripoti piya inaeleza kuwa nchi zenye utajiri wa mafuta, kama Urusi na Nigeria, ndio hasa kwenye mtindo wa fedha kutoweka na kuvushwa, badala ya kuwekezwa nchini.
Utafiti huo unamaliza kwa kusema wanasiasa sehemu mbalimbali za dunia, wanategemea kuwa fedha hata zikiwa kwa watu wa juu, zitavuja hatimae na kuwafikia maskini - ripoti inasema hayo hayatokei tena. kwa hisani ya bbc