Katika matukio ya kijamii, Zantel imetoa simu za mkononi 25 kwa manispaa
ya jiji la Arusha ili kuwarahisishia mawasiliano viongozi na watumishi wa
manispaa.Simu hizo ambazo zitasambazwa kwa Msitahiki Meya, Madiwani na
mkurugenzi wa mji, zitawarusu kupiga simu bure wakati wote kwa kutumia huduma
ya kipekee ya Zantel ya ‘CLOSED USER GROUP’.Akizungumza wakati wa makabidhiano
hayo, Mkurugenzi wa masoko wa Zantel, Bwana Deepak Gupta, alisema kampuni yake
ina mkakati madhubuti wa kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kusukuma
gurudumu la maendeleo. ‘Kwa simu hizi ambazo zina laini ya Zantel, watumishi wa
manispaa wanaweza kuwasiliana bure kabisa baina yao hivyo kurahisisha
mawasiliano na ushirikiano kwa vitengo mbambali vya manispaa pamoja na
kupunguza gharama’ alisisitiza Bwana Gupta.