.

SK FOUNDATION

SK FOUNDATION
SK Foundation ni shirika lisilo la kiserekali,lliloanzishwa rasmi  tarehe 2/8/2013 na ndugu Frank .A.Lyimo.SK Foundation ikibeba maana ya “SOMA KITABU FOUNDATION ”.Sababu kuu iliyo mfanya mmiliki wa  SK NETWORK,VIPEPERUSHI COMPANY NA HOME OF FIGURES  ndugu  FRANK .A. LYIMO  kuanzisha hii foundation ni kutokana na kundi kubwa la vijana wa kiafrika kutopendelea kusoma vitabu  kabisa.Hali hii imefanya bara letu kuwa nyuma kimaendeleo na kushindwa kukabili changamoto  mbali mbali za kisiasa na kijamii kutokana na uelewa mdogo wa mambo yanavyokwenda dunia.Ili kuweza kurudisha kuiokoa Afrika na hili janga la ukosefu wa maarifa ni jukumu letu sote kuhamasishana kusoma vitabu kwa wingi ili kupata  maarifa mpya kila wakati.Kutokana na  vijana ndio nguvu kazi kubwa ya taifa,ndio maana aliamua kuwahamasisha  vijana kusoma vitabu kwa nguvu zote ili waweze kupata maarifa na waweze kuyatumia kujenga taifa letu la Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Dhumuni la SK foundation
Dhumuni kuu la sk foundation ni kuhamasisha vijana wa Tanzania na waafrika kwa ujumla kusoma vitabu kila wakati kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.
Kauli mbio yetu
Soma kitabu ongeza maarifa.
MAWASILIANO
Tupo ubungo msewe
Dar es salaam
Fax  +255 736604852
Simu namba:+ 255 767 592224
                        +255 713 592224
Tovuti:         www.somakitabu.blogspot.com 
Kazi zetu
Kuhamasisha vijana kujenga tabia ya kusoma vitabu  kupitia mitandao ya kijamii na vipeperushi.
Kukusanya vitabu vinavyofaa kusomwa na vijana na kuvisambaza kwa vijana wote Tanzania na afrika
Kukutana na watunzi wa vitabu kwa mwaka mara mbili ili kuratibu sindano la usomaji vitabu
Kuihimiza serekali kusambaza vitabu kwa wingi kwenye maktaba,mashule na vyuo ili vijana wapate kuvisoma kwa urahisi
Kuhimiza serekali na wadau wengine kujenga maktaba za kisasa kila kona ya nchi ili vijana wapate sehemu bora na tulivu za kujisomea.
Kujiunga nasi
Unaweza  kujiunga nasi  na  tukafanya kazi pamoja ya kuhamasisha vijana kusoma vitabu kwa manufaa yao na ya taifa kwa ujumla.Tutumie  barua pepe yenye maelezo yote muhimu na  dhumuni la kutaka kujiunga nasi.
Kuchangia
Unaweza kuchagia mawazo,fedha au chochote kile unachoona kinafaa na kitasaidia kukuza na kuendeleza  shirika hili ili liweze kuwafikia vijana wengi na kutoa huduma kwa ufanisi zaidi.


    “ soma vitabu ongeza maarifa,okoa taifa”





Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...