.

DR ULIMBOKA APELEKWA NJE YA NCHI KWA MATIBABU ZAIDI

Kutokana na afya ya mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari kuendelea kuwa mbaya Jumuiya  ya madaktari  iliamua kumpeleka daktari huyo nje ya nchi ili aweze kupata matibabu zaidi kutokana na hospitali  umma  hapa nchi  kukosa vifaa muhimu ambavyo lati kama  vingekuwepo basi dokta asingepelekwa nje ya nchi.katika hatua nyingine hali ya utolewaji wa huduma imezidi kudhorota kupita kiasi kwenye hospitali za umma kutokana na mgomo wa madaktari kushika kasi na baadhi ya madaktari kufukuzwa kazi katika mikoa ya  mbeya,Mwanza na Kilimanjaro.
Serekali yatolewa nje
Katika hatua nyingine madaktari wamegoma kuchukua msaada wa serekali walioonyesha nia ya kutaka kumsaidia dr ulimboka gharama za matibabu nje ya nchi..wamesima wao kama madaktari na wadau wa afya pamoja na jamii imeshajipanga kusimamia matibabu ya dokta hivyo hawahitaji msaada kutoka serekalini.
Wananchi wasikitishwa
Wananchi mmoja ameaamua kuacha kuendesha pikipiki ambayo ndo iilikuwa biashara yake kwa kuhofia kuwa kama akipata ajali kipindi hiki cha mgomo basi angeshindwa kupata matibabu na kama ni kidonda kingeoza .wengine walisikika wakisema kuwa wanasiasa ndo wamewafikisha hapa kwa kuwa wanaleta siasa kwenye roho zao .Wakazidi kulaumu kuwa wamejiongezea posho wabunge na madiwani huku madaktari,wanafunzi,walimu  na wananchi  kwa ujumla wa kitaabika kwa matatizo mbali mbali ambayo yanaweza kutatuliwa kama wangeweka kipaumbele mambo ya muhimu kwanza.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...